01. Maudhui yetu


Maudhui yetu:
Kuhusiana na adabu za uulizaji, kuwauliza Wanazuoni, na haja kubwa iliyopo katika kujua adabu za kuwauliza maswali Wanazuoni.
Ni ipi njia ya kuwauliza!?
Na wanaulizwa mambo gani!?
Na swali huwaje!?
Na ni vipi hupokelewa jawabu!?
Na yale yote yanayompasa Muislam katika kuwaheshimu Wanazuoni na kutowafakamia kwa lukuki ya maswali ya ung’ang’anizi na mfano wa hayo.
Na ifahamike kuwa Wanazuoni waliotangulia walishaandika kwa wingi kuhusu mambo haya ya adabu (za uulizaji) katika vitabu vyao:
1. أدب العلم والتعلم
Adabu za elimu na utafutaji wake.
2.أدب الطالب مع شيخه
Adabu za mwanafunzi kwa sheikh wake
3.حقوق أهل العلم بعامة
Haki za Wanazuoni kwa watu wa kawaida wasiokuwa Wanazuoni.
Na Allaah aliyetukuka amesema kwenye kitabu chake:
والمؤمنون ولمؤمنات بعضهم أولياء بعض يأمرون بالمعروف وينهون عن المنكر
Al-tawbah:71
“Na waumini wakiume na waumini wakike baadhi yao wao kwa wao ni marafiki”.
Yaani: baadhi yao huwapenda wengine na kuwanusuru na kuondoleana vikwazo na shida.
Na katika waumini ambao wanastahiki kupendwa na kunusuriwa ni Wanazuoni, kwasababu Allaah amewataja sambamba na nafsi yake kwa kushuhudia juu ya upweke wake wa ibada, pale aliposema:
شهد الله أنه لا إله إلا هو والملائكة وأولوا العلم قائما بالقسط لا إله إلا هو العزيز الحكيم
Al-imran:18.
“Ameshuhudia Allaah kwamba hakuna mola apasayekuabudiwa kwa haki isipokuwa yeye.
Na Malaika na Wanazuoni pia wameshuhudia.
Na kwamba yeye ni msimamiaji uadilifu.
Hakuna mola apasayekuabudiwa kwa haki isipokuwa yeye, Mwenye nguvu Mwenye hekima”.
Hivyo Wanazuoni ndio wateule wabora mbele za watu.
Muhusika: Shaykh Swaalih Aalish-Shaykh
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: adabus-suaal uk.7
Imehaririwa: 10’jumaadal-uwlaa/1438H