01. Thawabu kwa mwenyekutawadha vyema kipindi cha baridi kali ilhali anapata mashaka


Imepokelewa kutoka kwa Jaabir bin Abdillaaah (Allaah amridhie), amesema, amesema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Hivi nisikujuzeni juu ya yale ambayo Allaah kupitia hayo hufuta makosa na kusamehe madhambi!
Wakasema ndiyo tujuze ewe Mtume wa Allaah!
Akasema:
“Ni kueneza maji ya udhu kwenye viungo wakati wa machukizo, na kukithirisha hatua kuelekea misikitini, na kuisubiri swala baada ya swala”.
ameipokea ibn Hibban na asili yake ipo kwenye sahihi Muslim.
Muhusika: duaatsalaftz.net
Marejeo: miirathun-Nabiyy uk.3
Imehaririwa: 25Rthaaniy/1438H