01.Yanayuhusu Swiyaam – Maana ya Swaum


Maana ya Swaum:

Swaum ki-Lugha ni kujizuia. Na ki-Istilahi ni kumuabudu Allāh kwa kujizuia kutokana na vyoye vinavyofunguza kuanzia wakati wa kuchomoza kwa alfajiri ya kweli mpaka kuzama kwa jua.
Na swaum ya Ramadhani ni moja ya Nguzo tano za Uislamu, atakayepinga uwajibu wake amekufuru. Na atakayewacha kufunga kwa kutojali tu huwa ni muovu miongoni mwa waovu. Na wamekwenda kimadhehebu baadhi ya Wanazuoni kuwa mtu huyo huwa ni murtadd aliyetoka katika Dini ya Kiislamu.

 

Muhusika: Shaykh Abdillāh Al-Jibriin(Allāh Amraham)
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Sharh ‘Umdatul-fiqh