02. Kama ambavyo Allaah amesema:


(يرفع الله الذين آمنوا منكم والذين أوتوا العلم درجات (المجادلة: 11
“Anawainua Allaah wale walioamini miongoni mwenu, na waliopewa elimu huwainua (wote hao) daraja nyingi”.
Hivyo Allaah aliyetukuka amewainua Waumini juu ya watu wote, amewainua daraja nyingi, na amewainua Wanazuoni katika Waumini juu ya wote wenye Imani kwa ujumla, hivyo wao ni watu wa kipekee na ndio wateule. Kwa sababu ya ule uelewa wao kwenye maneno ya Allaah na sunnah za Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) umezifanya nyoyo zao kuwa na nuru kubwa kuliko nyoyo za wasiokuwa wao.
Kwasabau nuru haipatikani ila kwa elimu, na nuru hupatikana kwa kuielewa Qur’aan na Sunnah.
Amesema Allaah:
(قد جائكم من الله نور وكتاب مبين (المائدة: ١٥
“Kwa hakika imekujieni kutoka kwa Allaah nuru na kitabu kibainishacho”.
Yeyote atakaeifahamu Qur’aan na kuifahamu Sunnah anakuwa na nuru kubwa moyoni, na anakuwa na haki kuu katika haki wanazopata watu wa Imani.
Na kinachoonekana ni kuwa mtu mwenyepupa ya kutaka kufanya jambo la kheri huwauliza Wanazuoni.
Anawauliza katika mambo ya kifiqhi yale ambayo yanamkabili, anawauliza mambo ya kijamii yanayomkabili miongoni mwa matatizo ya nyumbani kwake ,kazini na mfano wake.
Na anayejifunza pia humuuliza mwalimu.
Lakini tumeona kwamba mengi katika maswali yametoka nje ya mwelekeo unaopasa, kama vile kuwaheshimu Wanazuoni, kuwajali nakutotia dosari haki zao.
Utakuta miongoni mwa watu wanaingiza mambo yasiyofaa kwenye maswali yao wanapowauliza Wanazuoni.
Muhusika: Shaykh Swaalih Aalish-Shaykh
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: adabus-suaal uk.8
Imehaririwa: 11’jumaadal-uwlaa/1438H