02.Ujumbe kwa Wapenzi wa Ahlul-Bayt-01


Na huu ndio wakati wa kuanza kuutoa ujumbe na kuuweka mbele ya Wasomaji:
1- Ikiwa mafungamano baina ya watu wa karibu na nyumba ya Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) na Maswahaba wa Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam), na nyumba nyengine za Maquraysh yalikuwa mabaya yenye mifundo na kupigana kama vinavyotupa taswira hiyo vitabu vya shia, basi ni ipi siri iliyopo katika majina na ukweli ulioko baina ya watu wa nyumba ya Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam)-Ahlul-Bayt- na Maqurayash waliobakia miongoni mwa Maswahaba na waliokuja baada yao?
Mifano juu ya hilo:
a) Aliyy (Allāh amridhie) kuwaita wengi wa watoto wake na wajukuu kwa majina ya Maswahaba, hususan Abūbakr, ‘Umar, ‘Uthmān na Twalha (Allāh awaridhie).
Na miongoni mwa watoto (wake hao) ni:
▪Abūbakr bin ‘Aliyy
▪Abūbakr bin Al-Hasan.
Ambao waliuawa vitani pamoja na Al-Husein (Allāh amridhie). [1]
▪Abūbakr bin Al-Hasan
▪Al-Muthanna bin Al-Hasan Kijukuu, (Allāh amridhie).
▪Abūbakr bin Muwsā Al-Kādhim.
Na wapo (katika Ahlul-Bayt) waliojiita kwa kuniyah ya Abūbakr:
Miongoni mwa waliojiita hivyo ni ‘Aliyy Zaynul-‘Aabidiin bin Al-Husain Al-Shahiid, na Aliyy Al-Ridhā bin Muwsā Al-Kādhim.

 

 

————————
[1] الإرشاد للمفيد ص ١٨٦ ص ٢٤٨

 

 

Muhusika: El-Bāhithiin Fil-Muntaqaa
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Ilaa Muhibbiy Aalil-Bayt Uk. 4-5