02.Yanayuhusu Swiyaam – Fadhila za Swaum


Fadhila za Swaum:

 

Na zimekuja dalili nyingi zinazojulisha juu ya ubora wa swaum na fadhila zake. Miongoni mwa hizo ni kauli ya Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam):

كل عمل ابن آدم يضاعف، الحسنة عشر إمثالها إلى سبعمائة ضعف، قال الله عز وجل: {إلا الصوم فإنه لي وأنا أجزي به، يدع شهوته وطعامه من أجلي}. للصائم فرحتان: فرحة عند فطره، وفرحة عند لقاء ربه، ولخلوف فيه أطيب عند الله من ريح المسك.  متفق عليه

“Kila tendo la mwanaadamu hulipwa kwa nyongeza, jema kwa kumi mfano wake, mpaka nyongeza mia saba. Amesema Allāh mwenye Nguvu na Utukufu:
“Isipokuwa swaum, kwani hiyo ni yangu mimi, na Mimi ndiye Mlipaji wake, ameacha matamanio yake na vyakule vyake pamoja na vinywaji kwaajili yangu”.
Mfungaji ana furaha mbili: furaha wakati wa kufturu kwake, na furaha siku ya kukutana na Mola wake. Na harufu imtokayo kinywani mwake ni nzuri zaidi mbele za Allāh kuliko harufu ya miski” Bukhari na Muslim.

 

Muhusika: Shaykh Abdillāh Al-Jibriin (Allāh amraham)
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Sharh ‘Umdatul-fiqh