03.Dalili juu ya Uwajibu wa Tawhiidil-‘Ulūhiyyayh


2. Imewaamrisha waja juu ya Tawhiidil-Ibādah (kumuabudu Allāh  peke yake pasi na kumshirikisha na chochote), na ikawataka  walifanye hilo.  Kama alivyosema Allāh  Mtukufu:

وَاعْبُدُوا اللَّهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا”  النساء (٣٦)

“Na muabuduni Allāh  na wala msimshirikishe na chochote, na wazazi wawili muwatendee Wema”. Al-Nisā (36).

Na amesrma Allāh Mtukufu:

وَاعْبُدُوهُ وَاشْكُرُوا لَهُ ۖ ” العنكبوت (١٧)

“Na muabuduni peke yake na mshukuruni” Al-‘Ankabūt (17).

Na amesema Allāh Mtukufu:

وَأَنِ اعْبُدُونِي ۚ هَٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ ” يس (61)

“Na niabuduni peke yangu hii ndio Dini ya sawa” Yāsiin (61).

Na ayah nyenginezo.

3. Tawhiidil-Rubūbiyyah inalazimisha kuwepo kwa Tawhiidul-Uluuhiyyah.  Na hii ni njia ya kujenga hoja kwa vile vinavyotangulizwa. Kwani Qur’an hujenga hoja kwavyo.

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah

Kiunganishi: http://duaatsalaftz.net/category/makala/kitaabu-tawhiidil-ibaadah/

Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/

Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah

Imehaririwa: ‘6Jumaadal-Thāniy/1440H