03.Yanayuhusu Swiyaam – Yanayoharibu Swaum


Yanayoharibu swaum:

Ni wajibu kwa Muislam kujiepusha na yote yatakayofisidi swaumu yake, kama vile kufanya moja katika yale yanayovunguza, mithili ya kuachwa kuswali swala za faradhi wakati akiwa anaendelea na swaumu au mara tu anapomaliza.
Kwani kuacha swala ni kufuru inayomtoa mtu katika mila.
Na pindi Muislam anapoanguka katika ukafiri basi hupomoka matendo yake yote, iwe ni swaumu au mengineyo. Tunamuomba Allāh salama na afiya. Na watu kama hawa inawahusu ile kauli ya Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) aliposema:

رب صائم حظه من صيامه الجوع والعطش، ورب قائم حظه من قيامه السهر” رواه أحمد والدارمي (صحيح)

“Huwenda mfungaji asipate chochote kutoka katika swaumu yake zaidi ya njaa na kiu, na msimamaji (kwenye Qiyaam Layl) asipate chochote zaidi ya uchovu na mavune”. Ahmad na Al-Dārimiy.

 

 

Muhusika: Shaykh Abdillāh Al-Jibriin (Allāh amraham)
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Sharh ‘Umdatul-fiqh