04. Na amesema ibn ‘Abbas (Allaah awaridhie)


ما رأيت قوما خيرا من أصحاب محمد ﷺ ، ما سألوه إلا عن ثلاث عشرة مسألة حتى قبض كلها في القرآن، قد قال الله جل وعلا: (ويسألونك عن المحيض)، (وإذا سألك عبادي عني) إلى آخر هذه المسائل
“Sijapatapoona, watu ambao ni bora zaidi kuliko Swahaba wa Muhammad (swalla Llaahu ‘alayhi wasalla) , hawajamuuliza zaidi ya maswali kumi na tatu mpaka alipochukuliwa (kufariki).
Na yote yapo kwenye Qur’aan. Amesema Allaah:
“Wanakuuliza kuhusu hedhi (ni nini hukumu ya mwanamke akiwa katika hali hiyo)…”.
“Pindi watakapokuuliza waja wangu kuhusu mimi..”.
Jumla ya maswali waliyouliza Maswahaba kumuuliza
Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) pamoja na ukaribu waliokuwa nao kwake ni maswali kumi na tatu (tu). Na yote yapo kwenye Qur’aan.
Na walikuwa Swahaba (Allaah awaridhie), kutokana na kumheshimu kwao Nabiy (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) , na kuchukia kwao kumuuliza mara kwa mara, walipenda lau angekuja bedui kutoka ubeduini nje ya mji wa Madinah ili aje kumuuliza Nabiyy (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) , ili wafaidike kutokana na maswali na majibu yake.
Na imekuja pia hadithi nyengine sahihi:
“Hakika Allaah anachukia kwenu khabari za qiila wa
qaala (zisizojulikana vyanzo na kutokuwa na ithbati), na kuulizauliza sana, na kuzitupa mali (kwa jambo lisilo na faida)”.
[Bukhary na Muslim].
Na pia alisema Al-Hajjaj bin ‘Aamir Al-Thumaaliy , ya kwamba:
Hakika Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
إياكم وكثرة السؤال
“Nakutahadharisheni na kuulizauliza sana”.
Hivyo (hizi) hadithi zinajulisha juu ya kwamba kukithirisha kuulizaliuliza Wanazuoni hilo ni jambo linaloingia kwenye umakruhu (na uchukivu), ila yale mambo ambayo atahitajia mja ufumbuzi wake katika yale ambayo yatakuja huko mbeleni (kiubainifu) kwa vidhibiti vyake.
Muhusika: Shaykh Swaalih Aalish-Shaykh
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: adabus-suaal uk.10
Imehaririwa: 11’jumaadal-uwlaa/1438H