04. Thawabu za swala kwa ujumla


Imepokelewa kutoka kwa Abuu Maalik al-Ash-‘ariy (Allaah amridhie) amesema:
Amesema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Twahara ni nusu ya imani, na al-hamdulillaah hujaza mizani, na subhaanallaahi pamoja na al-hamdulillaah hujaza usawa wa mbingu na ardhi.
Swala ni nuru na sadaka ni dalili (ya imani ya mwenyekutoa sadaka), na subra ni mwangaza, na Qur’an ni hoja yako au hoja dhidi yako”.
Ameipokea Muslim (23).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mutarjim: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.3
Imehaririwa: 25R’thaaniy/1438H