04.Washirikina na Tawhiidil-Ulūhiyyah


1. Washirikina ambao wanawaabudu wengine pamoja na Allāh, hawakupinga kuwa Allāh  anaabudiwa, walichopinga wao ni kustahiki kuabudiwa peke yake pasi na wenziwe. Na wakasema kuwaambia wale wanaowalingania kunako neno (لا إله إلا الله) ya kwamba:

“Hivi anataka kujaalia waungu wote (hawa) kuwa ni mungu mmoja? Hakika hili ni jambo la  kustaajabisha sana” Swād (5).

2. Washirikina walikuwa wakifanya  shiriki kipindi cha raha na fanaka, na wanamfanyia ikhlas Allāh  katika ibada kipindi cha shida (na misukosuko). Kwa sababu wanajua kuwa hakuna mwenye kuweza kuwaondolea madhara waliyokuwa nayo  ila  Allāh pekee. Na kwamba wale waabudiwa wao hawawezi kuwanufaisha katika kuwaondolea madhara, wala hawana uwezo aina yoyote, wala pia hawawezi kudhuru.  Kama alivyosema Allāh  Mtukufu:

فَإِذَا رَكِبُوا فِي الْفُلْكِ دَعَوُا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ فَلَمَّا نَجَّاهُمْ إِلَى الْبَرِّ إِذَا هُمْ يُشْرِكُونَ (65)لِيَكْفُرُوا بِمَا آتَيْنَاهُمْ وَلِيَتَمَتَّعُوا ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ ” العنكبوت

“Pindi wanapopanda kwenye marikebu (safina na majahazi) humuomba Allāh wakiwa na ikhlas na kumtakasia Dini. Lakini pale anapowaokoa na kuwafikisha nchi kavu utawaona wakimshirikisha.

Na waendelee kukufuru kwa yale  tuliyowapa na wastarehe, kwani (ipo siku) watakuja kujua” ‘An-Kabuut (65). 

Na ayah nyinginezo.

3. Hivyo Washirikina wenye kuabudu masanamu na mizimu wanakiri kuwa waabudiwa wao kinyume na Allāh  ni viumbe, havimiliki kwa nafsi zao wala nafsi za wanaowaabudu dhara wala nufaiko, hawamiliki kifo uhai wala kufufua, hawasikii hawaoni wala hawawafai kwa chochote.  Na wanakiri kuwa Allāh ndiye aliyepwekeka kwa uumbaji, kuruzuku, kudhuru, kunufaisha na kuendesha mambo.  Juu ya kujua kwao kuwa wao na wale wanaowaabudu hawamiliki kitu.  Ndio maana Allāh  akawalazimisha kwa yale wanayoyakubali na kuyakiri:

“Basi kama ambavyo mnakiri na kukubali kuwa Allāh  amepwekeka kwa uumbaji basi pia inakulazimuni mumpwekeshe katika Ibada”.

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah

Kiunganishi: http://duaatsalaftz.net/category/makala/kitaabu-tawhiidil-ibaadah/

Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/

Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah

Imehaririwa: ‘6Jumaadal-Thāniy/1440H