06. Hali za muulizaji na muulizwa


Kuwauliza Wanazuoni na Ahludh-Dhikr kuna hali zake, na watu wana hitajio la kuuliza, lakini uulizaji kama uulizaji una zake hali:
(a) hali kutoka katika upande wa Muulizaji.
(b) hali kutoka katika upande wa muulizwa.
Muulizaji anapaswa kuchunga adabu ili muulizwaji afikie katika tawfiiq ya kutoa jawabu la haki -inshaa Allaah-
Itampasa muulizaji kuchunga baadhi ya mambo, miongoni mwayo:
uwazi wa swali
Miongoni mwa mambo ambayo yatampasa kuyachunga muulizaji , ni maswali yake kuwa na uwazi yasiwe na mgubiko, yaani swali alitengeneze kwa bayana kabla ya kuuliza.
Na katika yanayolahidhiwa ni kwamba wapo miongoni mwa Waislam ambao wanapojiliwa na swali kwenye akili zao , au kukumbwa tu na tatizo haraka utawaona wakiwaendea Wanazuoni na kuwauliza mubashara pasi na kulihudhurisha vyema lile jambo akili mwake .
Au mubashara anainua simu na kumuuliza ‘Aalim yaliyomtokea pasi na kuwa ameyahudhurisha vyema (akili mwake).
Hatari ni pale muulizwaji anapotaka kuchambuliwa na kuwekewa wazi baadhi ya maswala ,utakuta huyu muulizaji anajibu:
“Wallaahi mie sijui, ni fulani tu aliwahi kuniambia (kuniusia hili) mie sijui!”.
Muhusika: Shaykh Swaalih Aalish-Shaykh
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: adabus-suaal uk.13
Imehaririwa: 20’jumaadal-uwlaa/1438H