07.Hakika ya Tawhiid Al-Ilāhiyyah (Al-Ibādah)


  1. Ni ile Tawhiid ambayo Allāh kwa ajili yake ameteremsha Vitabu. Kama alivyosema Allāh Mtukufu:

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ ” الأنبياء (25)

“Na wala hatujamtuma kabla yako Mtume yeyote ila  tulimshushia Wahyi kuwa hakuna Mola apasayekuabudiwa kwa haki isipokuwa Mimi hivyo nipwekesheni katika Ibada” Al-Anbiyaa (25).

Na miongoni mwa vitabu vilivyoteremshwa ni:

  1. Tawrāt
  2. Injiil
  3. Zabūr
  4. Sahifa za Ibrāhiim
  5. Sahifa za Muwsā
  6. Al-Qur’ān.

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah

Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah