07. Thawabu za kuswali safu ya kwanza


Imepokelewa kutoka kwa Al-Baraa bin ‘Aazib (Allaah amridhie), amesema:
“Alikuwa Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) , anakuja pembeni ya safu akisawazisha sawa baina ya vifua vya watu na mabega yao (kwenye upangaji), na alikuwa akisema:
“Msikhtalifiane kwani zitakhtalifiana nyoyo zenu, hakika Allaah na Malaika wake wanawaswalia wanaoswali safu ya kwanza”.
ameipokea ibn Khuzaymah katiak sahihi yake (3/26) , na ameifanyia takhriij Al-Albaaniy katika ”sahihul-jaami’i” (7255).
Na imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Allaah amridhie), kwamba hakika Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Lau watu wangelijua yapatikanayo kwenye adhana na safu ya kwanza (katika malipo), kisha wasipate suluhisho (baada ya kiminyano chao) zaidi ya kupiga kura , basi wangepiga kura (nani aadhini na nani aswali safu ya kwanza)”.
Ameipokea Bukhary (615) na Muslim (337).
Muhusika: Ikthiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.4
Imahaririwa: 3’jumaadal-uwlaa/1438H