07.Ujumbe kwa Wapenzi wa Ahlul-Bayt-06


Ukwe na mchanganyiko wa nasaba baina ya Ahlul-Bayt na Maswahaba wengine (Allāh awaridhie), hasahasa ukoo wa Abūbakr na ukoo wa Al-Khattwab pamoja na ukoo wa Al-Zubair.
Ukwe huu umepatikana kwa wingi sana kama ambavyo machimbuko ya vitabu vya shia tegemewa vinavyotaja.
Na mfano wa hilo:
a) Kuolewa kwa Ummu Kulthuum bint wa Aliyy (Allāh amridhie) na ‘Umar bin Al-Khatwab (Radhi za Allāh ziwe juu yake). [1]
Hakika tendo la Aliyy kumuozesha bint yake kww ‘Umar (Allāh amridhie) halijulishi tu juu ya kina cha mafungamano pekee na umadhubuti wa mahaba baina ya pande mbili, Bali pia hujulisha juu ya kuwa Aliyy anaonelea kuwa ‘Umar bin Al-Khattwab ndiye mtu aliye bora zaidi na mwenyekustahiki kuwa kijukuu cha Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) ni mke kwake.
Na hili linakwenda kinyume kabisa na itikadi ya shia kwa ‘Umar (Allāh amridhie).
Na hebu fikiria kwa makini kauli yake Allāh Mtukufu:

“وَالطَّيِّبَاتُ لِلطَّيِّبِينَ وَالطَّيِّبُونَ لِلطَّيِّبَاتِ ۚ أُولَٰئِكَ مُبَرَّءُونَ مِمَّا يَقُولُونَ ۖ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ      ” النور 26

“Wazuri wakike ni wa Wazuri wa kiume, na Wazuri wa kiume ni wa Wazuri wakike, hao wako mbali kutokana na wayasemayo watu wazushi, na watapata msamaha na riziki nzuri ” Al-Nuur (26).

 

 

——————-
[1] الكليني فروع الكافي (١١٥/٦)، والطوسي في تهذيب الأحكام (باب عدد النساء ١٤٨/٨)

 
 
Muhusika: El-Bāhithiin Fil-Muntaqaa
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Ilaa Muhibbiy Aalil-Bayt Uk. 7-8