08. Inampasa muulizaji aliandae swali mwanzo kabisa


Na kwaajili ya hayo (tunasema), itampasa muulizaji alihudhurishe vyema (akilini mwake) swali, na aliandalie maneno mafupi yenye kueleweka, usidhani kuwa
muulizwa, muftiy, mwanafunzi aliyenauwezo wa kujibu maswali,
Usidhanie kuwa hao hupigiwa simu na mtu mmoja tu au wawili, siku hizi kwenye simu hizi huwa wapigao ndani na nje kuwapigia Wanazuoni kwa mwaka ni maelfu ya watu mathalan.
Na kwa siku moja huenda wakampigia watu ishirini au thalathini.
Hivyo katika adabu ambazo inapasa kuzichunga ni muulizaji aone ufinyu wa wakati wa muftiy (muulizwa), ufinyu wa wakati wa mjibuji maswali, hivyo ni juu yake kuliandaa swali kwa maneno machache yenye kueleweka ambayo hayana utata wala utandu.
Na ajitahidi kumsaidia Muftiy juu ya kumchungia muda wake ili pia maswali yake yalete tija.
Muhusika: Shaykh Swaalih Aalish-Shaykh
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: adabus-suaal uk.14
Imehaririwa: 20’jumaadal-uwlaa/1438H