09. Thawabu kwa mwenyekuswali katika msikiti Mtukufu (Makkah), na msikiti wa Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) pamoja na msikiti wa Palestina


Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Allaah amridhie) , amesema
Amesema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Swala itakayoswaliwa katika msikiti wangu huu ni bora zaidi kuliko swala elfu moja zitakazoswaliwa katika msikiti mwengine ukitoa msikiti mtukufu.
Na swala moja katika msikiti mtukufu ni bora zaidi kuliko swala laki moja (misikiti mingine)”.
Sahihi ameipokea Ahmad (3/343), ibn Maajah (406), na ameifanyia takhriij Al-Albaaniy katika “Ir-waaul-ghaliil” (4/341).
Na imepokelewa kutoka kwa Abdillaah bin ‘Amr (Allaah awaridhie), kutoka kwa Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam), amesema:
“Alipomaliza Sulayman bin Daud (‘alayhis-salaam) kujenga baytul-maqdis, alimuomba Allaah ampe hukumu ambayo itasadifu hukumu yake, na ufalme ambao hatoupata mwenginewe baada yake, na kwamba hatoujia msikiti huu yeyote kwa dhamira ya kuswali ndani yake ila yapukutike madhambi yake awe sawa na siku aliyozaliwa na mama yake”
Akasema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Ama mawili aliyoyaomba kwa hakika ameshapewa, na nataraji kuwa amepewa na la tatu”.
Sahihi: ameipokea Ahmad (2/176), Al-Nasaaiyy (2/34), ibn Hibban (1408), ibn Khuzaymah (1334), ibn Maajah (1633), Al-Haakim (1/30) na ameifanyia takhriij Al-Albaaniy katika “sahihi ibn Maajah” (1156).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.5
Imehaririwa: 3’jumaadal-uwlaa/1438H