09. Usidhani kuwa Masheikh ni wako peke yako


Kamwe usijekudhani kwamba huyu aliyejibu swali lako kwa njia ya simu katika Wanazuoni ni wako pake yako.
Bali itakidi kuwa wanaowauliza Wanazuoni kwa siku ni makumi ya watu nakuwa wanawauliza kila wakati.
Hivyo ni lazima kuchunga hali na kuwa na adabu kwa Wanazuoni kwa kufupisha maswali, na ukubali majibu kwa namna alivyoyaleta, kwani siku zote swali likiwa wazi na jibu huwa wazi vivyo.
Na ndio maana utaona maswali ya Jibriil (‘alayhis-salaam) aliyomuuliza Nabiy (‘alayhis-swalaat wassalaam) yalikuwa ni kielelezo tosha juu ya mng’ao wa maswali yaliyopelekea kupatikana mng’ao wa majibu.
Mfano aliuliza Jibriil (‘alayhis-salaam) kumuuliza Nabiy ( ‘alayhi swalaat wasallaam):
“Nikhabarishe kuhusu Uislam!?”.
Swali fupi lililowazi kabisa.
“Nikhabarishe kuhusu Iymaan!?”
“Nikhabarishe kuhusu Ihsaan!?”
Na kuhusu alama za kiyama alisema:
“Na ni zipi alama zake!?”
Na mfano wa hayo.
Hivyo , uwazi wa swali na uchache wa maelezo yake, tena kwa kuyahudhurisha kwa mchanganuo wake kabla ya kuuliza, hili (jambo) ni miongoni mwa adabu ambazo zinapasa kuchungwa.
Na mara nyingi huwa majibu (ya Wanazuoni) hayapo wazi kwasababu muulizaji hakulitengeneza vyema swali lake. Lau muulizaji angeliandaa vyema swali lake kisha akauliza bila shaka jawabu pia lingekuwa zuri lililowazi.
Muhusika: Shaykh Swaalih Aalish-Shaykh
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: adabus-suaal uk.15
Imehaririwa: 20’jumaadal-uwlaa/1438H