10.Fadhila na ubora wa Tawhiid- A


Hakika atakayeipatikanisha hii Tawhiid (katika maisha yake) ataingia peponi. Kama alivyosema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) katika hadithi ya ‘Ubādah bin Al-Swāmit (Allāh amridhie):

من قال أشهد أن لا إله إلا الله  وحده لا شريك له وأن محمدا عبده ورسوله وأن عيسى عبد الله ورسوله وابن أمته وكلمته ألقاها إلى مريم وروح منه  وأن الجنة حق وأن النار حق أدخله الله من أي أبواب الجنة الثمانية شاء

رواه الشيخان

” Yeyote atakayeshahadia kuwa hakuna Mola apasaekuabudiwa kwa haki isipokuwa Allāh  peke yake hana mshirika, na kwamba Muhammad ni mja wake na Mtume wake, na kwamba Issa ni mja wa Allāh  na mtoto wa kijakazi wake, na ni neno lake aliloliweka kwa Maryam na ni roho itokayo kwake, na kwamba pepo ni haki na moto ni haki, basi Allāh  atamuingiza peponi kupitia mlango wowote miongoni mwa milango minane autakao”.
Ameipokea Bukhari na Muslim.

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah