10. Kuacha kuuliza lijulikanalo jawabule


Miongoni mwa adabu ambazo inapaswa kuchungwa katika hali ya uulizaji swali ni kutowauliza Wanazuoni kuhusu jambo ambalo linajulikana jawabu lake.
Wapo baadhi ya wanafunzi au wale ambao wana macho kiasi fulani, utakuta ameshayafanyia upekuzi baadhi ya masuala na akaona kauli zilizopo kwenye masuala hayo, kisha utamuona anakuja kuuliza tena (kwa Wanazuoni), na atakapojibiwa kwa jawabu ambalo limeafikiana na moja ya zile kauli alizoziona utaona anaanza kuleta kauli kinzani.
Utamuona akiuliza: kauli hii dalili yake ni ipi!?
(au): dalili hii mbona imeshajeruhiwa!?
(au): kauli hii mbona imeshatolewa maelezo yake!?
(au): Baadhi ya Wanazuoni wamelisemea hili kwa hivi na hivi!
Hivyo (tuelewe kwamba) kuna tofauti baina ya kuuliza ili upate faida au ujifunze ilhali hujui, na baina ya kuuliza ili ufungue mjadala.
Na mtu ‘Aalim sio kazi yake hiyo.
Kama wataka kujadiliana naye mtaarifu tangu mwanzo kwamba nataka kujadiliana na wewe kwenye masuala fulani.
faida
Kuuliza jambo ambalo jawabu lake linafahamika ni sehemu katika kujionesha.
Kama ilivyopokelewa kwa Wakii’i bin Al-Jarraah (Allaah amrehemu):
Amesema Al-Khatwib Al-Baghdaadiy (Allaah amrehemu) katika “al-jaami’u liakhkaaq al-raawiy” (1971):
وليتق إعادة الإستفهام لما قد فهمه، وسؤال التكرار لما قد سمعه وعلمه، فإن ذلك يؤدي إلى إضجار الشيخ
“Na achunge (mwanafunzi) kuulizauliza kuhusu lile alijualo, na maswali ya kukaririka kwa lile ambalo alishalisikia (ufumbuzi wake) na kulijua, kwani hakika jambo hilo linapelekea kumkasirisha Shaykh”.
Muhusika: Shaykh Swaalih Aalish-Shaykh
Mtarjimu: duaatasalaftz.net
Marejeo: adabus-suaal uk.16
Imehaririwa: 23’jumaadal-uwlaa/1438H