11. Tofauti baina ya swali na mjadala


Ni nini maana ya mjadala?
Maana yake: ni mimi kujadiliana na wewe na kwenye majadiliano hayo ukajua niliyonayo na mimi nikajua uliyonayo mwisho ni kuifikia haki.
Na hili huwa halitakikani hasa pale ambapo haitochungwa adabu (na nidhamu) kwa Wanazuoni.
Kwasababu katika hilo hupatikana baadhi ya suluki za utovu wa nidhamu juu ya haki za Wanazuoni.
Isipokuwa ukiwa muwazi kuwa unataka mubadilishane elimu katika masuala fulani. Kama atakupa idhini katika kubadilishana huko hali itakuwa imebadilika kutoka katika kuuliza na kutaka kujua kwenda kwenye kuyapekuwa mambo kupambanuliana.
Na hili pia hupatikana kwa baadhi ya wanafunzi kwenye vikao vya kielimu. Utakuta kijana ana maarifa ya kujua jawabu lakini anaendelea kuuliza ili amjuze mwengine kwamba ameuliza swali zuri kabisa, na mfano wa hayo.
Wakati tulionao kipindi hiki ni mdogo sana haipaswi kuuliza mambo ambayo tumeshayaua (fat’wa yake).
Hebu tuwe tunauliza tusiyoyajua. Na ndio maana katika ambayo tunatakiwa kuyachunga na kuwa na adabu nayo ni kutouliza ila lile ambalo hulijui.
Kwasababu Allaah (jalla wa’alaa) amesema:
“Waulizeni wajuzi (Ahlul-Dhikr) mkiwa hamjui”.

Kama unajua usiulize, kwasababu elimu tayari unayo, na ujue kuwa wakati wa Mufty au ‘Aalim au Twaalib al-‘ilm unapaswa kutumika kwenye mambo mengine mengi.
Na yale (mambo) ya wajibu pia yanapunjika kwa muda wa waliowengi vipi ukiongezea juu ya hilo mshupalio wa maswali na mfano wake!!
Muhusika: Shaykh Swaalih Aalish-Shaykh
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: adabus-suaal uk.18
Imehaririwa: 24’jumaadal-uwlaa/1438H