12. Thawabu za kutembea kuelekea misikitini kipindi cha kiza


Imepokelewa kutoka kwa Abud Dardaa (Allaah amridhie), kutoka kwa Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) , kwamba hakika yeye amesema:
“Yeyote atembeaye kwenye giza kuelekea misikitini, atakutana na Allaah kwa nuru ya siku ya kiyama”.
Sahihi: ameipokea ibn Hibban katika “sahihi” yake (3044).
Imepokelewa kutoka kwa Sahl bin Sa’ad Al-Saa’idiyy (Allaah amridhie), amesema:
Amesema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Na wapewe bishara njema watembeao gizani wendao misikitini, kwamba watapa nuru timilifu siku ya kiyama”.
Ameipokea ibn Maajah (780), ibn Khuzaymah (2/377), Al-Haakim (1/212) na ameifanyia takhriij Al-Albaaniy katika “sahihi ibn Maajah” (632).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.6
Imehaririwa: 3’jumaadal-uwlaa/1438H