13. Ipo hali unaruhusika kumuuliza mwengine asiyekuwa yule wa kwanza


Ni pale jawabu lake litakapokuwa lina utata katika upande wa dalili, mtu ana baadhi ya maarifa kisha jawabu alilopewa likampa utata katika upande wa dalili anayoruhusa kumuuliza mwengine kwasababu hajakinai kwa jibu (alilopewa), si kwa lengo la kwamba haliendani na hali yake au ugumu wake lile jawabu au kutonasibiana, au kwamba anatafuta wakumpa wepesi. Bali ni kwa sura ya kuwa ametatizika je, kweli hii ni hukumu ya Allaah (-jalla wa’alaa) na hukumu ya Mtumewe katika suala hili au laa!? Na hilo ni kwa uelewa wake alionao kwa baadhi ya dalili kwamba zinakwenda kinyume na hilo.
Muhusika: Shaykh Swaalih Aalish-Shaykh
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: adabus-suaal uk.20
Imehaririwa: 24’jumaadal-uwlaa/1438H