13.Ujumbe kwa Wapenzi wa Ahlul-Bayt-12


(6)- Shia hawawezi kupinga kuwa Abūbakr na ‘Umar (Allāh awaridhie) walimpa kiapo cha utiifu Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) chini ya ule mti. Na kwamba Allāh alishasema kuwa amewaridhia na ameyajua yaliyomo mioyoni mwao, kama alivyosem Mtukufu:

“لَّقَدْ رَضِيَ اللَّهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ فَعَلِمَ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَنزَلَ السَّكِينَةَ عَلَيْهِمْ وَأَثَابَهُمْ فَتْحًا قَرِيبًا     ” الفتح18

“Hakika Allāh amewaridhia Waumini pale walipokupa wewe kiapo cha utiifu chini ya ule mti. Akayaona Allāh yaliyomo mioyoni mwao, akawateremshia utulivu na kuwalipa ushindi ambao upo karibu” Al-Fat’h (18).
Hivi itawezekanaje kwa mashia leo hii baada ya hili (alilolitaja Allāh), kuzikana khabari za Allāh Mtukufu! Kisha wakayadai ya kinyume chake!?
Kama kwamba wanasema:
“Mola wetu huwajui hawa kama tuwajuavyo sisi”!
 
 
Muhusika: El-Bāhithiin Fil-Muntaqaa
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Ilaa Muhibbiy Aalil-Bayt Uk. 11