15. Thawabu kwa atakayeketi msikitini sehemu aliyoswalia baada ya swala ya as-subhi akimdhukuru Allaah mpaka jua kuchomoza


Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Allaah amridhie) amesema:
Amesema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Yeyote atakayeswali (swala ya) alfajiri kwa jamaa’ah, kisha akaketi akiwa anamdhukuru Allaah mpaka jua lichomoze, kisha akaswali rakaa mbili, atapata ujira wa hijja na ‘umrah.
Akasema tena (Anas):
Amesema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Malipo yaliyotimu kabisa! Malipo yaliyotimu kabisa! Malipo yaliyotimu kabisa!”.
Tanbiih
Amesema Ibn Baaz -rahmatullaah ‘alayhi- “malipo yoyote yaliyokuja yakiwahusu wanaume,na wanawake nao wameingia , na malipo yoyote yatakayowahusu wanawake na wanaume wameingia ila lile ambalo litataja kwa umaalum wa jinsia moja miongoni mwa hizo mbili!!”
Ni hadithi hasan kwa shawaahid zake. Ameipokea Al-Tirmidhiy (586).
Imepokelewa kutoka kwa Jaabir bin Samurah (Allaah amridhie), amesema:
“Alikuwa Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) akimaliza kuswali swala ya al-fajiri hukaa mkao wa tarabbu’i katika majlisi yake mpaka jua likachomoza likiwa wazi”.
Sahihi: ameipokea Muslim (670), na riwaya ya Twabaraaniy (2/150) ameidhoofisha Al-Albaaniy katika (dha’iifu al-targhiib” (371).
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Allaah amridhie), amesema:
Amesema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Hakika tendo la mimi kukaa pamoja na watu wanaomdhukuru Allaah kuanzia swala ya asubuhi mpaka kuchomoza kwa jua, hilo linapendeza zaidi kwangu kuliko kuwaacha huru wanne katika watoto wa (nabii) Ismaa’iil (‘alayhis-salaam).
Na kukaa kwangu pamoja na watu wanaomdhukuru Allaah kuanzia swala ya laasiri mpaka kuzama kwa jua , hilo lapendeza zaidi kwangu kuliko kuwaacha huru watu wanne”.
Hasan: ameipokea Abuu Daud (3667), na ameifanyia takhriij Al-Albaaniy katika “al-sahiiha” (2916).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.7
Imehaririwa: 5’jumaadal-uwlaa/1438H