16. Thawabu za nyiradi za baada ya swala ya asubuhi na maghribi


Imepokelewa kutoka kwa Abuu Dharr (Allaah amridhie), amesema:
Amesema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Yeyote atakayesema kila baada ya swala ya alfajiri akiwa amekunja miguu yake (mkao wa tashah-hud), kabla ya kuzungumza chochote:
لاإله إلا الله وحده لا شريك له، له الملك وله الحمد، يحيى ويميت وهو على كل شيئ قدير،
“Hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, peke yake hana mshirika, ufalme ni wake na himdi zote, anahuyisha na kufisha, na yeye juu ya kila kitu ni Muweza”
Mara kumi,
Allaah atamuandikia mema kumi, na atamfutia mabaya kumi, na atamuinua daraja kumi (za thawabu),na atakingwa na mabaya siku nzima, na atakingwa kutokana na shetani, na hatopatwa na dhambi ambalo litaangamiza (mema yake) siku hiyo ila dhambi la ushirikina”.
Hasan kwa shawaahid zake: ameipokea Al-Tirmidhiyy (3474), na Al-Nasaaiyy katika ” amal-al-yawm wallaylah” (127).
Tanbiih
Nyiradi za kishari’ah zisomwe kwa lugha ya shari’ah.
Muhusika: Ikhtiyaari ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.7
Imehaririwa: 5’jumaadal-uwlaa/1438H