16.Ujumbe Kwa Wapenzi Wa Ahlul-Bayt-15


9- Kombozi za Kiislam zama za Abūbakr, ‘Umar na ‘Uthmān (Allāh awaridhie) zilikuwa ni nyingi mno. Miongoni mwazo ni kukombolewa kwa miji ya fursi, miji ya Shamu, Baytul-Maqdis, Misr, Afrika, miji ya Sindi na mengineyo.
Je, hilo linahesabika ni katika nusra za Allāh kwa Uislam au laa!?
Na je, anahesabikaje yule ambaye haya yalijiri katika kipindi cha ukhalifa wake, ni Khalifa mbaya na dhalimu?
Na vipi itakuwa hali ya wanajeshi waliokuwa chini ya uongozi wake?
Bila shaka watakuwa mfano wake, na kwamba wao ndio wanajeshi waliopambana vilivyo.
Na wala hatoweza kusahau shia kuwa miongoni mwa hawa wanajeshi ambao wameikomboa miji alikuwepo
1) ‘Aliyy
2) Al-Hasan
3) Al-Husain
4) Salman
5) Abū Dharr
6) ‘Ammār.
Allāh awaridhie wote.
Je wabora hawa wanapewa hukumu gani?[1].
______
[1] Kwa maana kwamba wale Makhalifa watatu walioikomboa miji na kuingiza Uislamu walikuwa ni makafiri vipi watakuwa wanajeshi wao?

 

 

Muhusika: El-Bāhithiin Fil-Muntaqaa
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Ilaa Muhibbiy Aalil-Bayt Uk. 18-20