17. Miongoni mwa Fadhila na Ubora wa Tawhiid- 3


 Kwamba ile Bitwāqah (card) itakayotolewa kupewa mja (siku ya kiyama) na ndani yake kuna Shahāda  ya لا إله إلا الله itatia uzito katika upande wa mizani na itaviinua vitabu (vya madhambi vilivyopo upande wapili wa mizani). Kama alivyosema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) katika hadithi ya ‘Abdullāh   bin ‘Amri (Allāh  amridhie):

فتخرج بطاقة فيها أشهد أن لا إله إلا الله وأشهد أن محمدا عبده ورسوله فيقول احضر وزنك فيقول يا رب ما هذه البطاقة مع هذه السجلات فقال إنك لا تظلم قال فتوضع السجلات في كفة والبطاقة في كفة فطاشت السجلات وثقلت البطاقة فلا يثقل مع اسم الله شيئ

رواه الترمذي وابن ماجة وأحمد والحاكم (صحيح)

“Itatolewa bitwāqah ndani yake ina kushahadia kuwa hakuna Mola apasayekuabudiwa kwa haki isipokuwa Allāh  na kwamba Muhammad ni mja wake na Mtume wake. Atasema (Allāh):
Hudhuria mizani yako.  Atasema (mja): Ewe Mola! Itafanya nini hii bitwāqah mbele ya vitabu vikubwa hivi?
Atasema (Allāh):
“Hakika hutodhulumiwa”
Anasema:
Vitawekwa vitabu kikubwa (vya madhambi) katika upande wa mizani na bitwāqah katika upande mwengine, vikainuliwa vile vitabu vikubwa  na upande wa bitwāqah ukawa mzito. Basi hakuna chochotw kitakachoshinda dhikri ya Allāh”.

 

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah