17. Thawabu za kuswali swala za sunnah nyumbani


Imepokelewa kutoka kwa zayd bin Thaabit (Allaah amridhie), kwamba hakika Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Swalini enyi watu majumbani mwenu, kwani hakika swala bora ya mtu ni ile aiswaliyo nyumbani kwake isipokuwa swala ya faradhi”.
Sahihi: ameipokea Al-Nasaaiyy (3/198), na ameifanyia takhriij Al-Albaaniy katika sahihi ya nasaaiy (1508).
Imepokelewa kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (Allaah amridhie), amesema:
Amesema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Atakapomaliza mmoja wenu swala msikitini kwake, basi na ajaalie sehemu ya swala nyumbani kwake, kwani hakika Allaah anajaalia nyumbani kwake kheri kwasababu ya swala zake”.
Sahihi: ameipokea Muslim (778).
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Muwsaa (Allaah amridhie), kutoka kwa Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Mfano wa nyumba ambayo hutajwa Allaah ndani yake, na nyumba ambayo hatajwi Allaah ndani yake, ni mfano wa aliye hai na aliye mfu”.
Sahihi: ameipokea Bukhary (6407).
Imepokelewa kutoka kwa Abdillaah bin Sa’d (Allaah amridhie), amesema:
“Nilimuuliza Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam), kipi ni bora, kuswali nyumbani kwangu au kuswali msikitini!?
Akasema:
“kwani huijui nyumba yangu!? Ina ukaribu kiasi gani na msikiti !?
Basi kuswali kwangu nyumbani hilo lapendeza zaidi kwangu kuliko kuswali msikitini isipokuwa (tu!) swala ya faradhi”.
Ameipokea Ahmad (4/342), na ibn Khuzaymah (2/210), na ibn Maajah (8731), na ameifanyia takhriij Al-Albaaniy katika “sahihi ibn Maajah” (1133).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miirathun-Nabiyy uk.7
Imehaririwa: 5’jumaadal-uwlaa/1438H