18. Thawabu kwa atakayedumu na rakaa kumi na mbili kwa mchana na usiku


Imepokelewa kutoka kwa Ummi Habiibah bint wa Abiy Sufyan (Allaah awaridhie), amesema:
“Nilimsikia Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam),akisema:
“Hakuna mja yeyote muislam atakayeswali kwaajili ya Allaah kila siku rakaa kumi na mbili za sunnah zisizo za faradhi, isipokuwa Allaah atamjengea nyumba peponi, au atajengewa nyumba peponi”.
Sahihi: ameipokea Muslim (728), na Al-Tirmidhiy (415).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.8
Imehaririwa: 6’jumaadal-uwlaa/1438H