20. Hili lilishawahi kutokea


Liliwahi kutokea hili (Sheikh kurikodiwa bila ya ridhaa), na alipoulizwa kuhusiana na fat’wa yake alikataa kwamba hakusema hivyo, bali jambo alilolifutu lina upambanuzi wake na melekezo.
Bila shaka swali na jawabu lililorikodiwa lilikuwa wazi kabisa, lakini kwanini amesema kwamba suala lina upambanuzi wake na maelekezo?
Ni pale alipojua kwamba sasa jambo limeingia sura nyengine ya kunakishiwa, lakini mwanzo kabisa alidhani pale alipoulizwa na muulizaji kwa njia ya simu kwamba suala halitomvuka huyu mtu na kwamba litaishia tu kwake.
Hivyo, miongoni mwa yapasayo kuyachunga kwa Wanazuoni – na kwa hakika tumeamrishwa kuwaheshimu kama ilivyokuja athar kutoka kwa idadi ya waliowengi katika mataabiina tumeamrishwa kuwaheshimu Wanazuoni- na miongoni mwa kuonesha heshima zetu kwao ni kutowarikodi kwa vinasa sauti au kimaandishi na kutawanya bila ya idhni yao.
Bali hata yale uyasikiayo kutoka kwake kipindi akisherehesha baadhi ya masuala ni lazima umuoneshe ayakubali ndo aidhinishe kutawanywa au kutolewa copy.
Ni lazima tuyafanye hayo, kwasababu lile ambalo (ameona) litawafaa watu fulani huenda kwake lisiwafae wengine walio wengi. Kwasababu waliowengi -katika watu- hutofautiana kwa daraja zao, huenda ‘Aalim akachunga hali za waliombele yake pale anapozungumza, lakini kama angejua kuwa haya ayazungumzayo yatatawanywa kwa jamii na kupokelewa kwa akili tofauti bila shaka huenda angetoa jawabu lengine lisilokuwa la kwanza.
Na ndio maana utaona baadhi ya maswali Wanaulizwa Wanazuoni kwa njia ya simu hutofautiana majibu yao lau wangeulizwa katika kipindi (nuurun’alad-darb), kwenye kipindi hiki majawabu yanakuwa na upambanuzi (mrefu), pia huwa na dalili na hoja na mfano wa hayo kwasababu kipindi kinarushwa hewani kwa jamii (ya Waislam).
Lakini wakikujibu wewe wanakujibu kwa jinsi ya hali yako ilivyo, watakijibu tu kuwa:
Yafaau /haifai
Yajuzu/haijuzu
Sunna ni kadhaa/
Yote hayo ni kwasababu wakati wao ni mfinyu hawawezi kutaja mambo kwa upambanuzi kwa kila mmoja atakayewauliza.
Muhusika: Shaykh Swaalih Aalish-Shaykh
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: adabus-suaal uk.28
Imehaririwa: 28’jumaadal-uwlaa/1438H