21. Thawabu za swala ya witri


Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (Allaah amridhie), amesema:
Amesema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Enyi watu wa Qur-aan! Swalini witri, kwani hakika Allaah ni mpweke (witrun-watrun) na anapenda witri (na kulipa juu yake)”.
Sahihi: ameipokea Abuu Daud (6141), na ameipokea Bukhary (7406) kutoka katika hadithi ya Abuu Hurayrah).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.8