24. Thawabu kwa atakayeswali swala ya dhuha na akadumu nayo


Imepokelewa kutoka kwa Abuu Dharr (Allaah amridhie), kutoka kwa Nabiy (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam), amesema:
“Hupambaukiwa na asubuhi kiungo cha kila mmoja wenu juu ya kutolewa sadaka, basi kila tasbihi moja moja ni sadaka, na kila tahlili ni sadaka, na kila takbiri ni sadaka, na kuamrisha jema ni sadaka, na kukataza ovu ni sadaka, na yote hayo hutoshelezwa na rakaa mbili (tu) ambazo ataziswali mtu wakati wa dhuha”.
Sahihi: ameipokea Muslim (720).
Imepokelewa kutoka kwa Buraydah (Allaah amridhie), amesema:
“Nimemsikia Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam), akisema:
“Katika mwili wa mwanaadamu kuna viungo (viungio/joint) mia tatu na sitini, hivyo ni juu yake akitolee sadaka kila kimoja.
Wakasema (Maswahaba):
“Na ni nani ambaye ataweza hilo ewe Nabii wa Allaah!?”, akaseama:
“Ni kohozi lililopo msikitini atakapolifukia, au kitu chochote (chenye kuudhi wapita njia) atakapokisogeza pembeni, na kama hutoweza (hayo) ,basi rakaa mbili za dhuha zitakutosheleza”.
Sahihi: ameipokea Ahmad (5/354), na Abuu Daud (5242), na ibn Hibban (2531), na ibn Khuzaymah (2/229), na ameisahihisha Al-Albaaniy katika “sahiih al-targhiib” (666).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.9
Imehaririwa: 9’jumaadal-uwlaa/1438H