26. Thawabu kwa yale atakayoyasema aliyefiwa


Imepokelewa kutoka kwa Ummu Salamah mke wa Nabiy (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) na radhi za Allaah ziwe juu yake , amesema:
Nimemsikia Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) , akisema:
“Hakuna mja yeyote atakayepatwa na msiba kisha akasema:
إنا لله وإنا إليه راجعون، اللهم اجرني في مصيبتي، واخلف لي خيرا منها
Hakika sisi (sote!) ni wa Allaah, Ewe Allaah! Nipe ujira katika msiba wangu huu, na unipe badali ya bora kuliko hiki.
Isipokuwa Allaah atamlipa (tu!) ujira wake na atampa badali ya bora kuliko hicho”.
Anasema (Ummu Salamah):
Alipokufa Abuu Salamah , nilisema:
“Muislam gani bora kuliko Abuu Salamah!?
(yeye) ni nyumba za mwanzoni zilizohama (kutoka makkah) kuhamia kwa Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam)!!
Kisha hakika mimi nikayasema hayo maneno .
Allaah akanipa badali kwa kunipa Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam)”.
Ameipokea Muslim na Al-Tirmidhiy , ila yeye amesema:
Alisema (Ummu Salamah):
Amesema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Pindi mmoja wenu atakapopatwa na msiba, na aseme:
إنا لله وإنا إليه راجعون، اللهم! عندك أحتسب مصيبتي، فأجرني بها، وأبدلني بها خيرا
Hakika sisi ni wa Allaah, Ewe Allaah! Kwako wewe natumai malipo ya msiba wangu, hivyo nakuomba unilipe, na unipe badali ya kheri kuliko huu”.
Sahihi: ameipokea Muslim (918), na Al-Tirmidhiy (3509).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.10
Imehaririwa: 9’jumaadal-uwlaa/1438H