29. Thawabu za mtumishi wa sadaka na mweka hazina


Imepokelewa kutoka kwa Abuu Muwsaa Al-ash-‘ariy (Allaah amridhie), kutoka kwa Nabiy (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Hakika mweka hazina aliye Muislam mwaminifu ambaye anatekeleza aliloamrishwa, akakitoa kikiwa kamili hali ya kuwa imeridhia nafsi yake, akakitoa kwa aliyeamuriwa kumpa, basi huyo atakuwa ni mmoja wa watoa sadaka “.
Sahihi: ameipokea Bukhary (1438), na Muslim (1023).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.10
Imehaririwa: 9’jumaadal-uwlaa/1438H