30. Shuruti za لا إله إلا الله


{Sharti yapili}

  1. Kuwa na yakini inayopingana na shaka.
Anatakiwa mwenyekuitamka awe na yakini ya kuwa hakuna mola anayepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allāh, tena yakini hiyo iwe ni yakukata shauri  asiwe na shaka yoyote katika hilo. Kama alivyosema Allāh Mtukufu:

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا

الحجرات ١٥

“Hakika si vinginevyo Waumini wakweli ni wale waliomuamini Allāh  na Mtume wake kisha hawakuingiwa na mashaka” Al-Hujurāt (15).
Ama akiwa na mashaka  basi atakuwa ni mnafiki na wala haitamfaa لا إله إلا الله. Kama alivyosema Allāh Mtukufu:

إِنَّمَا يَسْتَأْذِنُكَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَارْتَابَتْ قُلُوبُهُمْ فَهُمْ فِي رَيْبِهِمْ يَتَرَدَّدُونَ

التوبة 45

“Hakika si vinginevyo wanaokuomba wewe ruhusa (ya kutoshiriki Jihadi) ni wale wasiomuamini Allāh  na siku ya mwisho na mioyo yao ikawa imejawa na shaka wakawa  wametayahari katika shaka zao” Al-Tawbah (45).
Na amesema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) katika hadithi ya Abū Hurayrah (Allāh  amridhie):

أشهد أن لا إله إلا الله وأني رسول الله لا يلقى الله بهما عبد غير شاك فيهما إلا دخل الجنة

رواه مسلم

“Nakiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi kwamba hakuna mola anayepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allāh, na kwamba mimi ni Mtume wa Allāh, mja hatokutana na Allāh  kwa mawili haya akiwa hana mashaka  nayo isipokuwa ataingia peponi”.
Ameipokea Muslim.

 

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah