31. Shuruti za لا إله إلا الله


{Sharti ya tatu}

  1. Kuwa na Ikhlas inayopingana na shirki na unafiki pamoja na riyaa.
Na hilo ni yeye anatakiwa atende matendo (ya kiibada) akiwa anamtakasia Allāh kutokana na uchafu wa ushirikina. Kama alivyosema Allāh Mtukufu:

“وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ”  

البينة 5

“Na wala hawakuamrishwa ila  wamuabudu Allāh hali ya kumtakasia Dini (Ikhlās) wanyenyekevu walioielekea Tawhiid na kujiepusha na ushirikina, na wasimamishe swala na watoe zaka na hiyo ndio Dini ya sawa sawa” Al-Bayyinah (5).
Na amesema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) katika hadithi ya Abū Hurayrah (Allāh  amridhie):

“أسعد الناس بشفاعتي يوم القيامة من قال لا إله إلا الله خالصا من قلبه أو نفسه”

رواه البخاري

“Hakika atakayeufurahia zaidi Uombezi wangu siku ya kiyama ni yule aliyesema لا إله إلا الله akiwa na Ikhlās moyoni au nafsini mwake”.
Ameipokea Bukhari.

 

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net/
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah