35. Thawabu kwa atakayemfanyia wepesi mdeni (anayemdai), au akamuongezea muda (kulipa deni), au akamsamehe kabisa


Amesema Allaah aliyetukuka:
(وإن كان ذو عسرة فنظرة إلي ميسرة وأن تصدقوا خير لكم إن كنتم تعلمون (البقرة: ٢٨٠
“Na kama atakuwa yupo kwenye dhiki ya hali basi muongezeeni muda mpaka kipindi cha wepesi , na kama mtatoa sadaka (kwa kumsamehe deni) hilo ni bora zaidi kwenu lau mngelikuwa mnajua”.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Allaah amridhie) , kutoka kwa Nabiy (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Yeyote atakayemuondolea muumini tatizo miongoni mwa matatizo ya kilimwengu , Allaah (naye) atamuondolea tatizo katika matatizo ya siku ya kiyama.
Na yeyote atakayemfanyia wepesi aliyebanwa (na hali) hapa duniani, basi Allaah atamfanyia wepesi duniani na akhera.
Na yeyote atakayemsitiri Muislam (mwenzake) , atasitiriwa na Allaah duniani na akhera.
Na Allaah yupo tayari kumsaidia mja , muda wa kuwa mja yupo tayari kumsaidia nduguye”.
Sahihi: ameipokea Muslim (2699).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.12
Imehaririwa: 14’jumaadal-uwlaa/1438H