36. Thawabu za kukopesha


Ametaja kwa takhriij ibn Maajah na Al-Bayhaqiy kwa isnadi zao , kutoka kwa Anas bin Maalik (Allaah amridhie) , amesema:
Amesema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Niliona usiku wa Israa nilipochukuliwa, juu ya mlango wa pepo kumeandikwa:
الصدقة بعشر أمثالها ، والقرض بثمانية عشر
“Sadaka moja hulipwa kwa kumi mfano wake, na mkopo kwa kumi na nane”.
Sahihi: ameipokea Ahmad (4/296), na Al-Tirmidhiy (1957), na ibn Hibban (5074), na ameisahihisha Al-Albaaniy katika “al-mishkaat” (1917).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.12
Imehaririwa: 14’jumaadal-uwlaa/1438H