37. Thawabu kwa atakayefunga ramadhani kwa imani na kutaraji malipo


1. Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Allaah amridhie) , kutoka kwa Nabiy (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Yeyote atakayefunga ramadhani kwa imani na kutaraji malipo (kutoka kwa Mola wake), basi huyo atasamehewa yaliyopita katika madhambi yake (madogo)”.
Sahihi: ameipokea Bukhary (1901), na Muslim (759).
2. Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Allaah amridhie) , amesema:
Amesema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):
“Umekujieni mwezi wa ramadhani, mwezi uliojaa baraka, Allaah amekufaridhishieni kuufunga, hufunguliwa ndani yake milango ya mbingu (pepo), na hufungwa ndani yake milango ya moto, na hufungwa ndani yake vingunge vya mashetani, Allaah ndani yake ana usiku ni bora kuliko miezi elfu moja, atakayenyimwa usiku huo basi amenyimwa kheri zake (zilizo nyingi)”.
Sahihi: ameipokea Al-Nasaaiy (4/129), na Al-Bayhaqiy katika “al-shu’ab” (3600), na ameisahihisha Al-Albaaniy katika “al-mishkaat” (1962).
3. Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Allaah amridhie) , kwamba hakika Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Pindi iingiapo ramadhani, hufunguliwa kwa wingi milango ya pepo, na hufungwa milango ya moto, na hufungwa mashetani (yaani: viongozi wao)”.
Sahihi: ameipokea Bukhary (1898), na Muslim (1089).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.12
Imehaririwa: 14’jumaadal-uwlaa/1438H