39. Thawabu kwa atakayesimama katika usiku wa “laylatul-qadri” kwa imani na kutaraji malipo


Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Allaah amridhie) , kutoka kwa Nabiy (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Atakayesimama laylatul-qadri kwa imani na kutaraji malipo (kutoka kwa Allaah), atasamehewa yaliyotangulia katika madhambi yake”.
Sahihi: ameipokea Bukhary (1901), na Muslim (709), na Al-Nasaaiy (4/155).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.13
Imehaririwa: 14’jumaadal-uwlaa/1438H