41.Masāili muhimu yanayofungamana na kuihakikisha لا إله إلا الله


(b).   Mja aliyezihakikisha Shahādah mbili (uhakikisho wa wajibu) ni yule anayasimamia yote aliyoyawajibisha  Allāh  juu yake, kwa mujibu wa uwezo wake.  Na akajiepusha kutokana na yale aliyoyaharamisha  Allāh juu yake.
Na hakika amesema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam):

“فإذا نهيتكم عن شيئ فاجتنبوه وإذا أمرتكم بأمر فأتوا منه ما استطعتم”

رواه البخاري

“Basi ninapokukatazeni  jambo jiepusheni nalo.  Na ninapokuamuruni jambo liendeeni kadiri  ya uwezo wenu”.
Ameipokea Bukhari.

 

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah