46. Thawabu kwa atakayefunga jumatatu na alkhamis


Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Allaah amridhie), kwamba hakika Mtume wa Allaah (swall Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Huinuliwa matendo (ya waja) kila siku ya jumatatu na alkhamis, Allaah -‘azza wajalla- humsamehe katika siku hizo kila mja ambaye hajamshirikisha Allaah kwa chochote, isipokuwa mtu ambaye baina yake na nduguye wanamifundo (nyoyoni), husema (Allaah kuwaambia malaika wake):
“Waacheni wawili hawa mpaka wapatane”.
Na imekuja katika mapokezi mengine:
“Hufunguliwa milango ya pepo kila siku ya jumatatu na alkhamis, husamehewa waja wote ambao hawajamshirikisha Allaah kwa chochote, isipokuwa mtu ambaye baina yake na nduguye wanamifundo.
Husemwa:
“Wasubirieni hawa mpaka wapatane”.
Ila yeye amesema:
Hakika Nabiyy (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam), alikuwa akifunga jumatatu na alkhamis, akaulizwa :
Ewe Mtume wa Allaah! Hakika wewe unafunga kila jumatatu na alkhamis!
Akasema:
“Hakika siku ya jumatatu na alkhamis Allaah humsamehe katika siku hizo kila Muislam , ila wawili waliokatana (na kutengana), husema:
“Waacheni hao mpaka wapatane”.
Sahihi: ameipokea Muslim (2565) na ibn Maajah (1740).
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Merejeo: miiraathun-Nabiyy uk.14
Imehaririwa: 22’jumaadal-uwlaa/1438H