50. Thawabu kwa mwenyekujikimu katika hajj na ‘umrah


Imepokelewa kutoka kwa mama ‘Aaisha (Allaah amridhie) , kwamba hakika Nabiy (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) alimwambia kwenye ‘umrah yake:
إن لك من الأجر على قدر نصبك ونفقتك
“Hakika utapata ujira kwa kadri ya kuchoka kwako na (gharama za) kujikimu kwako”.
Ameipokea Al-Haakim (1/471) na ameisahihisha , na amemuafiki katika hilo Al-Dhahabiy.
Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.net
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.16
Imehaririwa: 22’jumaadal-uwlaa/1438H