52. Thawabu za matendo mema yatakayofanywa katika siku kumi za mwezi wa mfungo tatu


Imepokelewa kutoka kwa ‘Adbullaah bin ‘Al-‘Abbas (Allaah awaridhie) , amesema:

Hakika Nabiy (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:

“Hakuna siku ambazo matendo mema katika siku hizo yanapendeza zaidi kwa Allaah -‘azza wajalla- kushinda siku hizi”

Yaani: siku kumi za mwanzo.

Wakauliza:

Ewe Mjumbe wa Allaah! Hata jihadi katika njia za Allaah!?

Akasema:

“Hata jihadi katika njia za  Allaah (hazifikiii mema yatakayotendwa siku kumi za mwanzo wa mfungotatu), isipokuwa yule ambaye atatoka mwenyewe kwa nafsi yake na mali zake kisha kisirudi chochote katika hivyo”.

Na lafudhi yake nyengine katika moja ya mapokezi yake alisema:

“Hakuna jema lolote lililokubwa na takasifu mbele ya Allaah kuliko ‘amali njema atakayoitenda (mja) katika siku kumi za mfungotatu”.

Sahihi: ameipokea Bukhary (969), na Al-Bayhaqiy katika “al-shu’ab” (3752).

 

Muhusika: Ikhtiyaar ‘Ubayd

Mtarjimu: duaatsalaftz.net

Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.16

Imehaririwa: 23’jumaadal-uwlaa/1438H