55. Thawabu za kunywa maji ya Zamzam


ثواب شرب ماء زمزم

عن جابر رضي الله عنه ، أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((ماء زمزم لما شرب له)).

[حسن بشواهده: رواه أحمد (٣/٣٥٧) ، وابن ماجة (٣٠٦٢)، وخرجه الألباني في “الصحيحة” (٦٦٣)].

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (Allaah amridhie), kwamba hakika Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:

“Maji ya Zamzam ni kwa lengo la kunywewa kwake”.

Hasan kwa shawaahid zake:  ameipokea Ahmad (3/357), na ibn Maajah (3062), na ameifanyia takhriij Al-Albaaniy (Allaah amrehem) katika “al-swahiihah” (663).

faida

Maji ya Zamzam ni maji yenye baraka na ni chakula kama alivyosema Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) , na hadithi ipo kwenye sahihi Muslim.

Na wanazuoni waliifanyia kazi hii hadithi kuhusu maji ya Zamzam kwa dhumuni la kunywewa kwake..

Alisema Ibn Al-Qayyim (Allaah amrehem):

“Na kwa hakika nilijaribu mimi na wengine pia, kujiponya kwa maji ya Zamzam nikaona mambo yakustaajabisha -kabisa- na nilipona maradhi mengi kwa idhni ya Allaah” (Zaad).

Na kuhusu maji ya Zamzam amesema Al-Imam Al-Shawkaaniy (Allaah amrehem):

“Kauli yake Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam):

“Maji ya Zamzam ni kwa lengo la kunywewa kwake”

Ndani yake kuna dalili (hoja) juu ya kuwa maji ya Zamzam yanamnufaisha mnywaji kwa lengo lolote alilokunywa kwa ajili yake, liwe ni lengo la kidunia au kiakhera, kwasababu neno “ما” (lilikuja kwenye hadithi)  katika kauli yake لما شرب له

Ni miongoni mwa swiigha za kuenea. (Nayl).

Na Al-Imam Shaafiy (Allaah amrehem), aliyanywa maji ya Zamzam kwa madhumuni yake matatu.

  1. Awe na elimu.
  2. Awe na shabaha
  3. Aingie peponi.

‘Ulamaa wanasema , yote mawili alikuwa nayo, tunamtarajia kwa Allaah apate na latatu.  Rej:  “Al-Jawaahir” ya Shamsud Diin Al-Sakhaawiy.

 

Muhusika: Shaykh Ikhtiyaar ‘Ubayd

Mtarjimu: duaatsalaftz.net

Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.17

Imeheririwa: 20’jum-thaaniy/1438H