61.Kuwapenda Waumini na Kuwanusuru na Tahadhari Juu ya Kukhalifu Hilo-14


(n). Kuwa miongoni mwa wanaozoeleka na ndugu zao Waumini na katika wanaowanufaisha.
Na hakika Amesema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) katika hadithi ya Sahli bin Sa’ad (Allāh amridhie):

“المؤمن يألف ويؤلف ولا خير فيمن لا يألف ولا يؤلف”

رواه أحمد وزاد في حديث جابر رضي الله عنه:  وخير الناس أنفعهم للناس

“Muumini anatangamana na watu na yeye anazoeleka, na wala hakuna kheri kwa asiyetangamana na wenzake naye akawa hazoeleki”.
Ameipokea Ahmad. Na amezidisha katika hadithi ya Jābir (Allāh amridhie):
“Na mbora wa watu ni yule mwenye manufaa kwao”.
Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah