68. ​Thawabu kwa atakayesoma Suuratul-Baqarah​


   ​ثواب من قرأ سورة البقرة​

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:  ((لا تجعلوا بيوتكم مقابر، إن الشيطان يفر من البيت الذي يُقرأُ فيه سورةُ البقرة)).

[صحيح: رواه مسلم (٧٨٠)].

Imepokelewa kutoka kwa Abiy Hurayrah (Allaah amridhie) , kwamba hakika Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“Msizijaalie nyumba zenu  kuwa ni makaburi, hakika shetani anaikimbia nyumba ambayo husomwa ndani yake suuratul-baqarah”.
Sahihi: Ameipokea Muslim (780).

عن أبي إمامة الباهلي قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول:  ((إقرءوا سورة البقرة فإن أخذها بركة، وتركها حسرة، ولا تستطيعها البطلة)).

[صحيح: رواه مسلم (٨٠٤)].

Imepokelewa kutoka kwa Abiy Umaamah Al-Baahiliy (Allaah amridhie), amesema:
Nimemsikia Mtume wa Allaah (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) akisema:
“Isomeni suuratul-baqarah kwani hakika kuichukua kwake (kuihifadhi/kuisoma) ni baraka, na kuiacha kwake (kutoipatiliza/kuijali) ni majuto, na wala haiwezekaniki na wachawi”.
Sahihi: Ameipokea Muslim (804).
​faida​
Nyumba iliyomithilishwa na kaburi ni ambayo haisomwi Qur’an wala haiswaliwi ndani yake.
Na katika hilo pia kuna dalili ya kutofaa kuswali sehemu yenye kaburi iwe ni Msikitini au kwengineko, wala kusoma Qur’an makaburini ​Tahadhari!!​
Muhusika: Shaykh Ikhtiyaar ‘Ubayd
Mtarjimu: duaatsalaftz.et
Marejeo: miiraathun-Nabiyy uk.20-21
Imehaririwa: 3’shab/1438H