68.Kuwapenda Waumini na Kuwanusuru na Tahadhari Juu ya Kukhalifu Hilo-21


(u). Mtembelee ndugu yako na jumuika naye, na jaalia mapenzi yako kwake ni kwaajili ya Allāh.
Na imekuja katika hadithi ya wale watu saba ambao watafunikwa na Allāh katika kivuli chake siku ambayo hakutokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake hicho. Na akataja miongoni mwao kuwa ni:

“ورجلان تحابا في الله اجتمعا عليه وتفرقا عليه”

رواه الشيخان

“Na watu wawili waliopendana kwaajili ya Allāh wakajumuika juu yake na wakaachana juu yake”.
Ameipokea Bukhari na Muslim.
Na amesema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) katika hadithi ya Mu’ādh (Allāh amridhie):

“قال الله عز وجل وجبت محبتي للمتحابين في والمتجالسين في والمتزاورين في والمتباذلين في”

رواه أحمد

“Yamestahiki mapenzi yangu kwa wapendanao kwaajili yangu, wanaokaa kwaajili yangu, wanaotembeleana kwaajili yangu, na kupeana kwaajili yangu”.
Ameipokea Ahmad (sahihi).

 

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah