70.Kuwapenda Waumini na Kuwanusuru na Tahadhari Juu ya Kukhalifu Hilo-23


(w). Mtetee ndugu yako kwa kusimama upande wake mpaka aichukue haki yake kutoka kwa aliyemdhulumu. Na kama atakuwa yeye ndiye dhalimu basi mzuilie kutokana na kutenda dhulma.
Na hakika amesema Mtume (swalla Llāhu ‘alayhi wasallam) katika hadithi ya Anas (Allāh amridhie):

أنصر أخاك ظالما أو مظلوما، فقال رجل يا رسول الله أنصره إذا كان مظلوما أفرأيت إذا كان ظالما كيف أنصره قال تحجزه أو تمنعه من الظلم فإن ذلك نصره

رواه البخاري

“Mnusuru nduguyo akiwa dhalimu au mwenyekudhulumiwa. Akasema bwana mmoja: Ewe Mtume wa Allāh! Nitaweza kumnusuru akiwa anadhulumiwa, lakini ni vipi nitamnusuru akiwa yeye ndio dhalimu?
Akasema: Utamkinga au kumzuilia kutokamana na kuitenda hiyo dhulma, Kwani huko ndiko kumnusuru kwenyewe”.
Ameipokea Bukhari.

 

 

Muhusika: Muhammad bin Shāmiy Shaybah
Mtarjim: http://duaatsalaftz.net
Marejeo: Kitabu Tawhiidil-Ibādah